Sunday 30 September 2012

SIMBA YENDELEZA UBABE LIGI KUU BARA

Posted at  00:11  |  in  

JUMAPILI LAIVU SuperSport: YANGA v LYON 
Mabingwa watetezi Simba leo wameipiga Timu ya Magereza bao 2-1 na kuendeleza wimbi lao la ushindi kwa Mechi zao zote za Ligi Msimu huu wakielekea kucheza na Mahasimu wao wakubwa, Yanga, Mechi ifuatayo Jumatano inayokuja.
VPL_LOGOBao za Simba katika Mechi hii na Tanzania Prisons zilifungwa na Felix Sunzu na na Mrisho Ngassa baada ya kutanguliwa na bao la Prisons ambalo lilifungwa na Fupi.
Simba kwenye Mechi hii walipata pigo pale Mchezaji wao Amir Maftah alipotolewa kwa Kadi Nyekundu na hivyo yeye na Emmanuel Okwi, ambae amefungiwa Mechi mbili, wataikosa Mechi na Yanga hapo Jumatano Oktoba 3.
Kwenye Mechi nyingine ya Ligi, JKT Oljoro waliichapa Mgambo bao 3-1.
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumapili Septemba 30
Yanga v African Lyon [National Stadium, Dar es Salaam]
Jumatatu Oktoba 1
Ruvu Shooting v Mtibwa Sugar Sugar [[Azam Complex, Dar es Salaam]]]
Jumatano Oktoba 3
African Lyon v Toto Africans [[Azam Complex, Dar es Salaam]]]
Ruvu Shootings v Kagera Sugar[[Mabatini, Pwani], Pwani]
JKT Oljoro v Coastal Union          [[Sheikh Amri Abeid, Arusha], Arusha]
Yanga v Simba [National Stadium, Dar es Salaam]

Share this post

Kuhusu Mdaku Orijino

Tunafichua maovu, uozo na taka taka zoote wanazofanya watu wasio na staha. Unapicha yoyote habari yoyote ya washenzi wa tabia, tucheki tuwaanikeGoogle+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 BONGO MAGAZINE 1. by Mdakuzi
Proudly Powered by Blogger.
back to top