Thursday 5 September 2013

KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANIA MH. FREEMAN MBOWE ATOLEWA BUNGENI LEO NA KUSABABISHA VURUGU KATI YA WABUNGE WA UPINZANI NA ASKARI WA BUNGE

Posted at  05:49  |  in  skendo

Ni aibu nyingine ndani ya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania baada ya vurugu kubwa kutokea Bungeni leo, ambapo askari wa Bunge walikuwa wakivutana na Wabunge wa kambi ya upinzani waliokuwa wakipinga amri ya Naibu Spika ya kumtoa nje kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe.
Vurugu kubwa zimetokea Bungeni hivi sasa mara baada ya Naibu Spika kutoa amri ya kutolewa nje kwa kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni Freeman Mbowe ambapo wabunge wa kambi ya upinzani hawakukubaliana na amri hiyo.
Chanzo cha kutolewa kwa amri hiyo ni kutokana na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe kusimama na kuanza kuzungumza pasipo kupewa ruhusa ili apinge uamuzi wa kura zilizopigwa na Wabunge ambapo Bunge lilipiga kura ya kuuondoa mjadala wa mswada wa katiba au ubaki ambapo wabunge 56 walisema mjadala huo uondolewe na Wabunge 159 walisema mjadala huo uendelee kwani ulishapita kwenye hatua mbalimbali.
Mara baada ya zoezi la upigaji kura kuisha Naibu Spika Job Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge ambapo alimsimamisha Mhe. Mrema achangie mjadala na wakati huo huo Mhe. Mbowe naye alisimama kupinga uamuzi wa Naibu Spika na ndipo alipotoa amri kwa askari wa Bungeni wamtoe nje ya ukumbi wa Bunge na walifanikiwa kumtoa nje mara baada ya mvutano mkali kati ya Wabunge wa kambi ya upinzania dhidi ya polisi. Kwa maoni ya watanzania wengi imefika mahali ambapo ina bidi wabunge waweke maslahi ya taifa mbele. Hivi walichogomea upinzani kina maslahi yapi au hasara zipi kwa taifa? mmoja ya watazamaji wa bunge alihoji. Kuna mambo yanahitaji busara na uelewa ili maafikiano ya hoja yafikiwe aliongeza. Imefika mahali ushabiki usio na tija kwa watanzania tuachane nao. Hata hivyo bunge liliendelea na mjadala wa muswada wa marekebisho ya sheria ya utungwaji katiba mpya. 
Wakati huohuo mbunge wa vunjo mh. Mrema akichangia hoja hiyo ameweka wazi kwanini yeye hakutoka jana wala leo wakati kambi ya upinzani ikitoka bungeni. Mh. Mrema amesema yeye yupo bungeni kuwawakilisha wananchi wa vunjo na watanzania hivyo haoni busara kutoka nje na kuacha hoja ya msingi.

Share this post

Kuhusu Mdaku Orijino

Tunafichua maovu, uozo na taka taka zoote wanazofanya watu wasio na staha. Unapicha yoyote habari yoyote ya washenzi wa tabia, tucheki tuwaanikeGoogle+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 BONGO MAGAZINE 1. by Mdakuzi
Proudly Powered by Blogger.
back to top