Posted at 05:12 |  in
Hizi ndo picha za mji wa ORDOS uliopo China, mji huu umekua mji wa maajabu na umebatizwa jina la 'GHOST CITY'.
|
Baadhi ya mitaa ikiwa tupu katika mji huo |
Mji huu ni mji wa pili kwa ubora wa miundombinu na majengo baada ya ule
mji wa Beijing na ulijengwa kwa muda wa mwaka mmoja tu, mji huu
ulijengwa mwaka 20... baada ya mtikisiko wa kiuchumi ulipoikumba dunia
kiujumla, Serikali ya China iliamua kuujenga mji huu ili kuyanusuru
makampuni ya ujenzi ya chini kutokana na mtikisiko wa Uchumi uliokuwepo
kipindi hicho kwa kuyapa tenda ya kuujenga mpaka kukamilika. Tazama
Picha zake Hapa, hizi ni baadhi tu ya picha zipo nyingine nyingi zaidi..
|
Nyumba nyingi hizi zote hazina wakaaji |
|
Baadhi ya Majengo yaliyopo katika mji wa Ordos |
|
Mitaa ikiwa tupu bila watu |
Kitu cha ajabu ambacho kinafanya huu mji uitwe Ghost City ni ile hali
yake ya kutokuwa na wakaazi, Mji una kila kitu lakini idadi ya watu
wanaoishi katika mji huo ni ndogo sana, na hii inatokana na ukali wa
maisha katika mji huo, watu wengi wamepanga nyumba katika mji huo lakini
hawajaanza kuishi huko kwa kukwepa gharama kubwa za
maisha..........Tanzania ina mpango wa kujenga mji mpya wa kigamboni
kuanzia 2011-2030, hebu linganisha na wenzetu....wao wamejenga huo mji
ambao ni mkubwa sana zaidi ya miji mingine huko china kwa mwaka
mmoja.....sie KIGAMBONI itachukua miaka 20!! Speed yetu inaridhisha
kweli???????? Na je, KIGAMBONI nayo haitageuka kuwa GHOST CITY???? Maoni
yako please
Kuhusu Mdaku Orijino
Tunafichua maovu, uozo na taka taka zoote wanazofanya watu wasio na staha. Unapicha yoyote habari yoyote ya washenzi wa tabia, tucheki tuwaanikeGoogle+.
0 comments: