Tuesday 30 October 2012

Kimbunga Sandy kusababisha vifo vya watu 13 nchini Marekani

Posted at  07:57  |  in  siasa

 


 


 Kimbunga Sandy kikiendelea kupiga majiji nchini Marekani baada ya kutoka Carribean na kupiga Canada

Kimbunga cha Sandy kimeenda sambamba na kumiminika kwa theluji kwenye maeneo mengi nchini Marekani kitu ambacho kimeongeza ugumu kwa wananchi ambao wanahama makazi yao kupisha madhara ambayo yanaweza kujitokeza kutokanana na kimbunga hicho.
Miundombinu ikiwa ile ya barabara imeharibiwa vibaya kutokana na maji kujaa kwenye majiji mbalimbali nchini Marekani huku serikali wa Washington ikiendelea kutoa tahadhari kwa wananchi kuondoka kwenye maeneo ambayo yapo karibu na Pwani.
Kimbunga Sandy kabla hakijapiga nchi za Canadana na Marekani tayari kilishasababisha vifo vya watu sitini na saba katika eneo la Carribbean na hofu imeongezeka nchini Marekani idadi ya vifo inaweza ikaongezeka kutokana na kutokea maporomoko. Majiji ambayo yameathirika zaidi ya kimbunga cha Sandy ni pamoja na New York, New Jersey, Pennsylvania, Maryland, West Virginia na North Carolina ambapo Maofisa wameendelea kuwasihi wananchi kuondoka kwenye makazi yao.
Kimbunga hiki kimeathiri kampeni za uchaguzi wa urais nchini Marekani ambapo kwa mara ya pili Rais Barack Obama na hasimu wake Mitt Romney wamelazimika kusitisha harakati zao za kunadi sera zao kupisha watu kuondoka kwenye makazi yao. Rais Obama naye ametumia fursa aliyoipata akiwa Washington kutoa wito kwa wananchi kutii amri ambazo zinatolewa na Mamlaka husika kuhusiana na taarifa za mwenendo wa kimbunga zinavyotolewa.
Shughuli nyingi zimetatizika ikiwemo kufungwa kwa shule na kuahirishwa kwa safari za ndege na reli kutokana na kujiepusha na madhara ambayo yanaweza kutokea kutokana na kuendelea kwa kimbunga cha Sandy. Kimbunga cha Sandy kimesababisha vinu vya nyuklia vilivyopo New Jersey kuzingirwa na maji na tayari tahadhari imetolewa ya watu kukaa mbali kwani kama ikivuja isije ikaleta athari.

Share this post

Kuhusu Mdaku Orijino

Tunafichua maovu, uozo na taka taka zoote wanazofanya watu wasio na staha. Unapicha yoyote habari yoyote ya washenzi wa tabia, tucheki tuwaanikeGoogle+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 BONGO MAGAZINE 1. by Mdakuzi
Proudly Powered by Blogger.
back to top