Tuesday, 2 August 2016

MO AANZA AMWAGA HELA MSIMBAZI

Posted at  11:14  |  in  

Kuonyesha mapenzi yake makubwa na klabu, bilionea Mo Dewji ameipatia Simba kitita cha shilingi milioni mia moja kwa ajiliya usajiliMfanyabiashara anayetaka kuwekeza kwenye klabu ya Simba Mohamed Dewji 'MO' leo ameukabidhi uongozi wa timu hiyo Sh milioni mia moja kwa ajili ya kusaidia usajili.MO amesema kuwa hiyo ilikuwa ni moja yaahadi zake kutokana na mapenzi aliyokuwa nayo kwenye klabu hiyo kubwa nchini."Hata kama uongozi hawata ridhia mabadiliko ya Mimi kuwekeza billion 20 kwa kupewa hisa 51 haina shida nimetoa pesa hizo kwa mapenzi yangu na Simba," amesema MO.Uongozi wa Simba ulimuomba msaada bilionea huyo kuwapa hela za usajili ili waweze kusajili wachezaji wazuri watakapoifanyia mambo makubwa timu hiyo.Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amewatuliza wanachama wa klabu hiyo nakwa kuwataka kuwa na subira na swala wanalo litaka la mabadiliko ndani ya klabu hiyo chini ya mwekezaji Mohamed Dewji ‘MO’ watalipitisha.Aveva ameiambia Goal, wameona wapitishe mabadiliko hayo baada ya kugundua yana tija kubwa kwa klabu yao katika uendeshaji na hata kurudisha mafanikio ya timu hiyo hivyo muda si mrefu watapitisha mpango huo na kuwaafahamisha wanachama wao.“Tunatarajia kukutana na MO, kwa ajili ya kuweka sawa mambo flaniflani na ninaamini baada ya kikao hicho mambo yote yatakuwa sawa na tutamkabidhi tajiri huyo asilimia 51, ya hisa ili aweze kuiendesha timu na kutupa mafanikio kama ambavyo aliahidi,” amesema Aveva.Rais huyo nusura apigwe na wanachama hao Jumapili kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo baada ya kugoma kuipitisha agenda ya 9, ambayo ilikuwa inazungumzia mabadiliko, kwa klabu hiyo kukabidhiwa Mohamed Dewji.

Share this post

Kuhusu Mdaku Orijino

Tunafichua maovu, uozo na taka taka zoote wanazofanya watu wasio na staha. Unapicha yoyote habari yoyote ya washenzi wa tabia, tucheki tuwaanikeGoogle+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 BONGO MAGAZINE 1. by Mdakuzi
Proudly Powered by Blogger.
back to top