Posted at 08:29 |  in
nje
MANCHESTER-UINGEREZA,
Sir Alex Ferguson ametangaza kustaafu kuifundisha Manchester United baada ya miaka 27 ndani ya Old Trafford.
Taarifa
za Fergie kutaka kustaafu zilianza kuzagaa tangu jana mchana na usiku
zikazidi lakini hakuna habari yoyote rasmi iliyotoka United mpaka leo
asubuhi.
Ferguson aliwasili kazini kama kawaida asubuhi akiendesha
gari lake katika uwanja wa mazoezi wa United wa Carrington mnamo saa
kumi na mbili.
Akitangaza uamuzi wake wa kustaafu alisema: "Uamuzi huu nimeufikiria sana na sikukurupuka. Ni muda sahihi.
'Ilikuwa
ni muhimu kuiacha taasisi hii ikiwa katika hali nzuri na imara na
ninaamini nimefanya kazi nzuri sana. Ubora wa kikosi hiki kilichoshinda
ligi, na uwiano wa umri wa wachezaji unaonyesha kutaendelea kuwepo na
mafanikio katika hatua ya juu - mfumo mzuri wa kukuza vipaji unatoa
picha nzuri ya mafanikio ya siku zijazo ya klabu.
'Kutokea hapa,
nina furaha kuchukua majukumu ya ukurugenzi na ubalozi wa klabu hii.
Sasa naangalia mbele kuzitendea haki kazi zangu.
'Lazima niipe
shukrani familia yangu, mapenzi yao na sapoti imekuwa muhimu sana
kwangu. Mke wangu Cathy amekuwa mtu muhimu katika maisha yangu yote,
kunipa moyo pale mambo yalipokuwa hayaendi sawa na kunisapoti. Maneno
hayatoshi kuelezea namna gani wakati huu ulivyo kwangu.
'Kwa
wachezaji wangu na wafanyakazi wengine wa klabu, wa sasa na zamani,
ningependa kuwashukuru kwa kazi nzuri tuliyofanya pamoja iliyonisaidia
kuleta kumbukumbu nyingi za ushindi zisizosahaulika. Bila mchango wao
historia ya klabu hii kubwa isingekuwa tajiri kiasi hiki.
'Katika
miaka yangu ya mwanzo hapa, utetezi wa bodi kwangu, na Sir Bobby
Charlton zaidi, ulinipa hali ya kujiamini na muda wa kujenga timu ya
soka.
'Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, familia ya
Glazer imenipa kila kitu nilichohitaji katika kuiongoza Manchester
United kwa ubora wote na nimekuwa nina bahati sana kuweza kufanya kazi
na mtu mwenye kipaji na mwaminifu kama CEO David Gill, Nina washukuru
sana.
'Kwa mashabiki, shukrani sana. Mapenzi na sapoti mliyonipa
miaka yote siwezi kuielezea. Imekuwa ni heshima kubwa sana kuweza
kuiongoza klabu yenu na nimekuwa na ufahari wa muda wangu kama kocha wa
Manchester United." alimaliza Ferguson.
(CHANZO:SHAFFIH DAUDA,BBC)
Kuhusu Mdaku Orijino
Tunafichua maovu, uozo na taka taka zoote wanazofanya watu wasio na staha. Unapicha yoyote habari yoyote ya washenzi wa tabia, tucheki tuwaanikeGoogle+.
0 comments: