Chini ya Meneja Tito Vilanova,
aliembadili Pep Guardiola, Barcelona wana Pointi 18 na wamefunga bao 17
na kufungwa 5 tu kwenye Mechi zao 6 za Ligi.
Licha ya kushinda Supercopa mwanzoni mwa
Msimu baada ya kuifunga Barca bao 2-1 katika Mechi ya pili baada ya
kuipoteza ya kwanza kwa 3-2 huko Nou Camp, Mabingwa Real Madrid, chini
ya Kocha machachari Jose Mourinho, wamejikuta wakianza kampeni yao ya
kutetea Taji lao la Liga kwa kulegalega kufuatia kufungwa na Sevilla na
Getafe, na sare na Valencia, na kuwaacha Wadau wao wakitoa sababu
kibao za kudorora huko.
Wengine wanadai ‘kutokuwa na furaha’ kwa
Nyota wao Cristiano Ronaldo kumechangia, wengine wanasema ‘bifu’ la
Mourinho na Zinedine Zidane aliekuwa Mkurugenzi wa Ufundi kumechangia
huku kukiwa na ‘bifu’ jingine kati ya Mourinho na Sergio Ramos.
Lakini, kwa lolote lile, Real Madrid wanahitaji ushindi kwenye El Clasico hii au watajikuta wako Pointi 11 nyuma ya Barcelona.
Zipo dalili njema kwao kwa Timu yao
kuanza kubadilika hivi sasa huku Ronaldo akipiga hetitriki mbili
mfululizo, ile ya kwenye ushindi wa 5-1 dhidi ya Deportivo La Coruna na
ile ya juzi kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI walipoichapa Ajax huko Amsterdam
bao 4-1.
Lakini Barcelona wakishinda Mechi hii ya Jumapili litakuwa pigo kubwa kwa Real ambao watakuwa Pointi 11 nyuma.
0 comments: