Manchester City na Arsenal zinaingia
kwenye Mechi hii zikiwa na rekodi sawa kwenye Ligi Kuu England Msimu huu
kwa kushinda Mechi 2 na Sare 2 kwa kila mmoja lakini mara ya mwisho kwa
Timu hizi kukutana ilikuwa Mwezi Aprili na Arsenal kuibuka kidedea kwa
bao 1-0.
Hali za Wachezaji
Kiungo wa Manchester City Samir Nasri
huenda akaikosa Mechi hii dhidi ya Klabu yake ya zamani baada ya kuumia
musuli kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONS LEAGUE waliyofungwa 3-2 na Real
Madrid Jumanne iliyopita huko Santiago Bernabeu.
Lakini Man City watakuwa nao Sergio Aguero na Mario Balotelli baada ya kupona.
Arsenal goalkeepeitamkosa Kipa Wojciech Szczesny na itabidi Vito Mannone acheze badala yake.
Pia Arsenal itacheza bila ya majeruhi
wao wa muda mrefu, Jack Wilshere na Emmanuel Frimpong, licha ya
Wachezaji hao kuanza mazoezi baada ya kupata nafuu.
Tathmini
Katika Mechi 4 za Ligi washapiga bao 9
lakini Man City wameonyesha udhaifu kwenye Difensi ambayo haijatulia na
hubadilishwa mara kwa mara na Kocha Roberto Mancini.
Arsenal walianza Ligi Msimu huu kwa
kutofunga bao katika Mechi mbili na kuanza gumzo la pengo lililoachwa na
Robin van Persie aliehamia Man United lakini katika Mechi zao 3
zilizopita Arsenal washafunga jumla ya bao 10 kupitia Gervinho na Lukas
Podolski huku Kiango mpya Santi Cazorla aking’ara sana.
Hadi sasa Man City imeshacheza Mechi 31 za Ligi bila kufungwa wakiwa nyumbani kwao Etihad.
Uso kwa Uso
Man City wameifunga Arsenal katika Mechi 4 kati ya 5 walizocheza mwisho nyumbani kwa City.
Katika Mechi 4 za mwisho walizokutana, Kadi Nyekundu 4 zimeshatembezwa na 3 zilikuwa kwa Wachezaji wa Man City.
0 comments: