Monday 8 October 2012

VPL: YANGA YAPIGWA KAGERA 1-0

Posted at  10:59  |  in  bongo

SASA WASHIKA NAFASI YA 8!!


VPL_LOGOYanga leo huko Uwanja wa Kaitaba, Bukoba walipigwa bao 1-0 na Kagera Sugar na kuporomoshwa hadi nafasi ya 8 katika Mechi pekee ya Ligi Kuu Vodacom huku ushindi huo ukiupaisha Kagera Sugar hadi nafasi ya 3 kwa kufikisha Pointi 10 wakiwa nyuma ya Azam wenye Pointi 13 na vinara Simba wenye 16.
Bao la ushindi kwa Kagera Sugar lilifungwa katika Dakika ya 68 na Themi Felix.
Mechi hii ya Kagera Sugar na Yanga ilikuwa ichezwe jana lakini kutokana na Uwanja wa Kaitaba kuwa na shughuli nyingine za kijamii ikaahirishwa hadi leo.
Mechi ifuatayo kwa Yanga ni huko Mwanza dhidi ya Toto Africans Siku ya Alhamisi Oktoba 11.
MSIMAMO:
1 Simba Mechi 6 Pointi 16
2 Azam FC Mechi 5 Pointi 13
3 Kagera Sugar Mechi 6 Pointi 10
4 Prisons Mechi 6 Pointi 9 [Tofauti ya Magoli 1]
5 Coastal Mechi 6 Pointi 9 [Tofauti ya Magoli 0]
6 JKT Oljoro Mechi 6 Pointi 9 [Tofauti ya Magoli 0]
7 Mtibwa Sugar Mechi 5 Pointi 8 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Yanga SC Mechi 6 Pointi 8 [Tofauti ya Magoli 1]
9 Toto African Mechi 6 Pointi 7 [Tofauti ya Magoli 0]
10 Ruvu Shooting Mechi 6 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli -2]
11 African Lyon Mechi 6 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli -5]
12 JKT Ruvu Mechi 6 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli -7]
13 JKT Mgambo Mechi 6 Pointi 3
14 Polisi Moro Mechi 6 Pointi 2

Share this post

Kuhusu Mdaku Orijino

Tunafichua maovu, uozo na taka taka zoote wanazofanya watu wasio na staha. Unapicha yoyote habari yoyote ya washenzi wa tabia, tucheki tuwaanikeGoogle+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 BONGO MAGAZINE 1. by Mdakuzi
Proudly Powered by Blogger.
back to top