Sunday 14 October 2012

HABARI ZA MICHEZO WIKEND HII

Posted at  09:42  |  in  

KOMBE la DUNIA: Jumanne Spain v France

>>Iniesta ndani kwa Spain!!
>>FRANCE yapagawishwa kufungwa na Japan!!
ARMADILLO-STANDARDJumanne, Mjini Madrid, Mabingwa wa Dunia na Ulaya, Spain, wanaikaribisha France kwenye Mechi ya Kundi I la Kanda ya Ulaya kusaka nafasi kucheza Kombe la Dunia Mwaka 2014 na kitu pekee kinachomuumiza kichwa Kocha wa Spain, Vicente Del Bosque, ni nani ampange wakati France wao wameweweseka baada ya kuchapwa bao 1-0 na Japan kwenye Mechi ya Kirafiki hivi juzi.
Juzi, wakicheza Stade de France Mjini Paris, France walifungwa bao 1-0 na Japan katika Mechi ya Kirafiki, kwa bao lililofungwa mwishoni na hicho ni kichapo cha kwa kwanza kwa Kocha Didier Deschamps tangu aitwae Timu kutoka kwa Laurent Blanc mara baada ya kutolewa kwenye Robo Fainali ya EURO 2012 walipochapwa na Spain.
France watakwenda huko Madrid bila ya Viungo wa Wakabaji, Abou Diaby na Rio Mavuba, ambao wameumia lakini pia kitu kinachowapa fadhaa ni kuendelea kwa ukame wa magoli kwa Straika wao Karim Benzema ambae amefunga bao 15 tu katika Mechi 53 alizochezea Spain.
Kwa Spain, hali ni murua hasa baada ya kushinda ugenini katika Mechi yao ya pili ya Kundi I walipoitandika Belarus bao 4-0 na kutwaa uongozi wa Kundi hilo kwa tofauti ya magoli mbele ya France.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
KUNDI I
1 Spain Mechi 2 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli 5]
2 France Mechi 2 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli 5]
3 Georgia Mechi 3 Pointi 4
4 Finland Mechi 2 Pointi 1
Belarus Mechi 3 Pointi 0
+++++++++++++++++++++++
Kocha wa Spain, , Vicente Del Bosque, ambae alimchezesha Kiungo Sergio Busquets kama Sentahafu na kumpa namba Kiungo wa Arsenal, Santi Cazorla, kwenye Mechi na Belarus, anatarajiwa kufanya mabadiliko kwa ajili ya Mechi na France na kumweka Raul Albiol kama Sentahafu na pia kumchezesha Kiungo Andres Iniesta ambae hakucheza na Belarus.
Mechi hii ya Jumanne kati ya Spain na France inazikutanisha Timu zote zenye Pointi 6 kila mmoja na kila Timu inataka ushindi ili kupita moja kwa moja kwenda Fainali za Kombe la Dunia kama Mshindi wa Kundi.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Spain: Iker Casillas; Alvaro Arbeloa, Sergio Ramos, Raul Albiol, Jordi Alba; Sergio Busquets, Xabi Alonso, Pedro, Xavi, Andres Iniesta, Cesc Fabregas
France: Hugo Lloris; Mathieu Debuchy, Laurent Koscielny, Mamadou Sakho, Patrice Evra; Moussa Sissoko, Yohan Cabaye, Blaise Matuidi; Franck Ribery, Karim Benzema, Jeremy Menez
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Oktoba 16
[SAA za BONGO]
Albania v Slovenia
Andorra v Estonia
Belarus v Georgia
Belgium v Scotland
Bosnia-Hercegovina v Lithuania
Czech Republic v Bulgaria
Hungary v Turkey
Iceland v Switzerland
Israel v Luxembourg
Latvia v Liechtenstein
Macedonia v Serbia
Portugal v Northern Ireland
Romania v Netherlands
Russia v Azerbaijan
San Marino v Moldova
Slovakia v Greece
Spain v France
Ukraine v Montenegro
2000 Cyprus v Norway
2100 Faroe Islands v Rep of Ireland
2130 Austria v Kazakhstan
2130 Croatia v Wales
2145 Germany v Sweden
2145 Italy v Denmark
2200 Poland v England
FAHAMU:
-ULAYA yapo Makundi 9
-Washindi 9 wa kila Kundi wataingia Fainali moja kwa moja na Washindi wa Pili 8 bora wenye rekodi nzuri dhidi ya Timu zilizomaliza nafasi za Kwanza, Tatu, Nne na Tano kwenye Kundi lao watapelekwa kwenye Droo kupanga Mechi 4 za Mchujo, zitakazochezwa nyumbani na ugenini, ili kupata Timu nne zitakazoingia Fainali.
 

Wayne Rooney ataka Ukepteni wake England uwe wa kudumu

Jumapili, 14 Oktoba 2012 18:29
Chapisha Toleo la kuchapisha
WAYNE_ROONEY-KEPTENIStraika wa England Wayne Rooney amesema angependelea itokee Siku awe Kepteni wa kudumu wa Timu ya Taifa ya England baada ya kuiongoza vyema kama Kepteni wa Timu hiyo hapo juzi ilipoitwanga San Marino bao 5-0 huku yeye akipiga bao mbili.
Rooney, Miaka 26, alishika wadhifa huo wa Ukepteni kwa muda kwenye Mechi hiyo baada ya Nahodha wa England, Steven Gerrard, kutokuwepo kufuatia kutumikia Kifungo cha Mechi moja.
Rooney ametamka: “Ukiwa mdogo unaota kuichezea England na ukiichezea kinachofuata ni kutaka kuwa Nahodha!”
Rooney alianza kuichezea England akiwa na Miaka 17 hapo Mwaka 2003 na juzi Ijumaa amefikisha Mechi 77 za kuichezea England.
Bao zake mbili za hiyo Ijumaa zimemfanya afikishe bao 31 akiwa ni wa 5 kwa ufungaji bao nyingi kwa England na sasa amewapiku Nat Lofthouse, Sir Tom Finney na Alan Shearer.
Meneja wa England, Roy Hodgson, amekiri kuwa Rooney anastahili kuwa Kepteni na ipo Siku hilo litatimia.
MATOKEO:
ULAYA-Mechi za Makundi Kombe la Dunia 2014
Ijumaa Oktoba 12
Russia 1 Portugal 0
Finland 1 Georgia 1
Armenia 1 Italy 3
Faroe Islands 1 Sweden 2
Kazakhstan 0 Austria 0
Albania 1 Iceland 2
Czech Republic 3 Malta 1
Liechtenstein 0 Lithuania 2
Turkey 0 Romania 1
Belarus 0 Spain 4
Bulgaria 1 Denmark 1
Moldova 0 Ukraine 0
Slovakia 2 Latvia 1
Estonia 0 Hungary 1
Netherlands 3 Andorra 0
Serbia 0 Belgium 3
Greece 0 Bosnia-Hercegovina 0
Rep of Ireland 1 Germany 6
Wales 2 Scotland 1
England 5 San Marino 0
Luxembourg 0 Israel 6
Macedonia 1 Croatia 2
Switzerland 1 Norway 1
Slovenia 2 Cyprus 1
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Oktoba 16
Albania v Slovenia
Andorra v Estonia
Belarus v Georgia
Belgium v Scotland
Bosnia-Hercegovina v Lithuania
Czech Republic v Bulgaria
Hungary v Turkey
Iceland v Switzerland
Israel v Luxembourg
Latvia v Liechtenstein
Macedonia v Serbia
Portugal v Northern Ireland
Romania v Netherlands
Russia v Azerbaijan
San Marino v Moldova
Slovakia v Greece
Spain v France
Ukraine v Montenegro
2000 Cyprus v Norway
2100 Faroe Islands v Rep of Ireland
2130 Austria v Kazakhstan
2130 Croatia v Wales
2145 Germany v Sweden
2145 Italy v Denmark
2200 Poland v England
FAHAMU:
-ULAYA yapo Makundi 9
-Washindi 9 wa kila Kundi wataingia Fainali moja kwa moja na Washindi wa Pili 8 bora wenye rekodi nzuri dhidi ya Timu zilizomaliza nafasi za Kwanza, Tatu, Nne na Tano kwenye Kundi lao watapelekwa kwenye Droo kupanga Mechi 4 za Mchujo, zitakazochezwa nyumbani na ugenini, ili kupata Timu nne zitakazoingia Fainali.
 

VPL: Simba bado ipo juu lakini Azam yaja!!

Jumapili, 14 Oktoba 2012 17:56
Chapisha Toleo la kuchapisha
VPL_LOGOKwenye Ligi Kuu Vodacom, baada ya Simba kuvutwa shati ilipotoka sare na Coastal Union ya 0-0 Uwanjani Mkwakwani huko Tanga na Azam FC kuitungua Polisi Moro huko Morogoro, Mechi zote zikichezwa Jumamosi, Simba bado wapo kileleni wakiwa na Pointi 17 lakini Azam wamebaki nafasi ya Pili, Pointi moja nyuma, huku wakiwa na Mechi moja mkononi.
Nafasi ya 3 imeshikwa na JKT Oljoro wakiwa na Pointi 12 wakifuata Yanga wenye 11.
Ligi itaendelea tena Jumatano.
MSIMAMO:
1 Simba Mechi 7 Pointi 17
2 Azam FC Mechi 6 Pointi 16
3 JKT Oljoro Mechi 7 Pointi 12
4 Yanga SC Mechi 7 Pointi 11 [Tofauti ya Magoli 3]
5 Kagera Sugar Mechi 7 Pointi 11 [Tofauti ya Magoli 2]
6 Coastal Mechi 7 Pointi 10
7 Prisons Mechi 7 Pointi 9 [Tofauti ya Magoli 0]
8 Ruvu Shooting Mechi 7 Pointi 9 [Tofauti ya Magoli -1]
9 Mtibwa Sugar Mechi 6 Pointi 8
10 Toto African Mechi 7 Pointi 7 [Tofauti ya Magoli -2]
11 JKT Ruvu Mechi 7 Pointi  [Tofauti ya Magoli -7]
12 JKT Mgambo Mechi 7 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli -4]
13 African Lyon Mechi 7 Pointi 6 [Tofauti ya Magoli -6]
14 Polisi Moro Mechi 7 Pointi 2
RATIBA:
Jumatano Oktoba 17
Tanzania Prisons v Azam [Sokoine, Mbeya]
Polisi Morogoro v JKT Ruvu [Jamhuri, Morogoro]
Simba v Kagera Sugar [National Stadium, Dar es Salaam]
Mgambo JKT v Toto Africans [Mkwakwani, Tanga]
JKT Oljoro v African Lyon [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Jumamosi Oktoba 20
Yanga v Ruvu Shootings [Azam Complex, Dar es Salaam]
Coastal Union v Mtibwa Sugar [Mkwakwani, Tanga]
Jumapili Oktoba 21
JKT Ruvu v JKT Oljoro [Azam Complex, Dar es Salaam]
Mgambo JKT v Simba [Mkwakwani, Tanga]
Tanzania Prisons v Toto Africans [Sokoine, Mbeya]
 

KOMBE la DUNIA: Higuain hatihati kucheza na Chile

Jumapili, 14 Oktoba 2012 17:11
Chapisha Toleo la kuchapisha
>>ARGENTINA kileleni huko Marekani ya Kusini!!
BRAZIL_2014_BESTStraika wa Real Madrid Gonzalo Higuain ameumia mguu na yupo kwenye hatihati kama atachea Mechi ya Mchujo Kanda ya Marekani ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil hapo Jumatano dhidi ya Chile baada ya kupata majeruhi hayo kwenye Mechi ya Ijumaa ambayo Nchi yake Argentina iliifunga Uruguay bao 3-0.
Katika Mechi hiyo bao za Argentina zilifungwa na Lionel Messi, bao mbili, na Sergio Aguero.
Hadi sasa Argentina ndio wapo kileleni mwa Kundi hilo wakiwa na Pointi 17 kwa Mechi 8 na wapinzani wao wa Jumatano, Chile, wapo nafasi ya 5 wakiwa Pointi 5 nyuma yao.
========================
MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 13
Ecuador 3 Chile 1
Argentina 3 Uruguay 0
Ijumaa Oktoba 12
Bolivia 1 Peru 1
Colombia 2 Paraguay 0
RATIBA:
Jumatano Oktoba 17
Bolivia v Uruguay
Venezuela v Ecuador
Paraguay v Peru
Chile v Argentina
MSIMAMO KANDA ya NCHI za MAREKANI ya KUSINI:
Timu zote zimecheza Mechi 8
1 Argentina Pointi 17
2 Colombia 16
3 Ecuador 16
4 Uruguay 12
5 Chile 12
6 Venezuela 11
7 Peru 8
8 Bolivia 5
9 Paraguay 4
FAHAMU: Timu 4 za juu zinatinga Fainali Brazil moja kwa moja na ile ya 5 itaenda Mechi ya Mchujo.
 

AFCON 2013: Mabingwa Zambia wapita kwa matuta!

Jumapili, 14 Oktoba 2012 07:35
Chapisha Toleo la kuchapisha
>>Ghana, Mali, Nigeria, Sierra Leone, Morocco zipo Fainali!!
AFCON_2013-NORMALMabingwa watetezi Zambia, ambao walishinda 1-0 katika Mechi ya kwanza, wametinga Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, licha ya kupigwa bao 1-0 hapo jana huko Kampala na wameibuka Mshindi kwa Mikwaju ya Penati 9-8.
Bao la Uganda lilifungwa na Geofrey Massa katika Dakika ya 27.
Timu nyingine zilizofanikiwa kutinga Fainali zitakazochezwa huko Afrika ya Kusini kati ya Januari 19 na Februari 10, Mwakani ni Ghana, Mali, Nigeria, Sierra Leone na Morocco.
Mechi kati ya Ivory Coast na Senegal ilivunjika katika Dakika ya 76.
Leo zinaendelea kuchezwa Mechi nyingine zitakazotoa Washindi wengine kujumuika na Wenyeji Afrika Kusini.
MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 13
Malawi  0 : 1 Ghana [Ghana wamepita]
Botswana 1 : 4   Mali [Mali wamepita]
Uganda 1 : 0 Zambia [Zambia wamepita Penati 9-8]]
[Bao: 27' Geofrey Massa]
Nigeria  6 : 1 Liberia
Tunisia  0 : 0 Sierra Leone [Sierra Leone wamepita]
Senegal v Ivory Coast [Mechi imeahirishwa]
Morocco 4 : 0 Mozambique [Morocco wamepita]
Jumapili Oktoba 14
[SAA za Bongo]
[Matokeo Mechi ya kwanza kwenye mabano]
2000 Algeria v Libya [1-0]
1700 Cameroon v Cape Verde [0-2]
1830 Togo v Gabon [1-1]
1800 Angola v Zimbabwe [1-3]
1800 Niger v Guinea [0-1]
1600 Ethiopia v Sudan [3-5]
2100 Burkina Faso v Central African Republic [0-1]
2100 E.Guinea v Congo DR [0-4]
FAHAMU: Washindi 15 wa Mechi hizi watajumuika na Wenyeji Afrika Kusini kwenye Fainali zitakazochezwa Afrika Kusini Januari 2013.

Share this post

Kuhusu Mdaku Orijino

Tunafichua maovu, uozo na taka taka zoote wanazofanya watu wasio na staha. Unapicha yoyote habari yoyote ya washenzi wa tabia, tucheki tuwaanikeGoogle+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 BONGO MAGAZINE 1. by Mdakuzi
Proudly Powered by Blogger.
back to top