.
Jeshi la Polisi Arusha
limekanusha taarifa zilizoenea toka jana kwamba watu wanne walifariki
October 21 2012 baada ya fujo kutokea kwenye Pub Lamonte Karatu ambayo
ilitangaza kwamba Barnaba angeimba lakini baadae mashabiki wakagundua
waliibiwa viingilio kwa sababu hakua Barnaba orijino.
Taarifa nilizozipata usiku huo
kutoka kwa mwandishi wa habari wa Mlimani Tv ziliamplfy kwamba mauaji
hayo yalitokana na ugomvi wa chupa na visu.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha
amesema hakuna mauaji yoyote yaliyotokea usiku huona kwamba amepigiwa
simu nyingi sana na waandishi wa habari wakiulizia hizo taarifa.
Mmoja kati ya watu
walioshuhudia ambae pia alilipa kiingilio kumuona Barnaba amesema kweli
fujo zilitokea na watu walimpiga chupa yule Barnaba feki baada ya
kumgundua ni muongo na alikua hawezi kuimba nyimbo za Barnaba kwenye
stage, alikua anajikanyaga kanyaga kabla ya kuokolewa na mabaunsa kwa
kutolewa kwenye hiyo pub.
Shahidi huyu aitwae Ibrahim
amesema ukumbi ulikua na watu wasiopungua 200 na mpaka sasa
hawajarudishiwa viingilio vyao na wala mmiliki hana time nao na wala
hajapatikana uizungumzia hii ishu.
Kwa mujibu wa Ibrahim, hii ni
mara ya pili kwa Pub hiyo kupeleka msanii feki… wa kwanza alikua Ally
Kiba ambae watu waligundua wameibiwa lakini hawakufanya chochote, millardayo.com bado inamtafuta mmiliki wa hiyo Pub ili kupata stori kamili.
posted by Millard Ayo website.
0 comments: