Tuesday, 23 October 2012

ALEX FERGUSON NA RIO WAMALIZA MZOZO.

Posted at  02:07  |  in  nje




.
Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema ameshayamaliza na mchezaji wake Rio Ferdinand ambae weekend iliyopita kwenye game na Stoke City aligoma kuvaa t-shirt ya kampeni ya kupinga ubaguzi wa rangi kwenye soka ambapo ndio alikua mchezaji pekee ambae hakuvaa t shirt ya hiyo kampeni.
Fergie amesema aliaibika kutokana na hicho kitendo cha Rio lakini baadae aligundua ilitokana na tatizo la mawasiliano ila kwa sasa tayari ameshafanya nae mazungumzo hivyo sio ishu kubwa tena manake wameyamaliza ambapo Fergie amesema pia kwamba Rio ataongezewa mkataba wa mwaka mmoja baada ya huu wa sasa kuisha.
Ukiachia Rio Ferdinand ambae mdogo wake Anthony Ferdinand wa QPR alikua na ishu ya ubaguzi kutoka kwa John Terry hivi juzi, zaidi ya wachezaji 30 kwenye Premier League wamepinga hiyo kampeni.

Share this post

Kuhusu Mdaku Orijino

Tunafichua maovu, uozo na taka taka zoote wanazofanya watu wasio na staha. Unapicha yoyote habari yoyote ya washenzi wa tabia, tucheki tuwaanikeGoogle+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 BONGO MAGAZINE 1. by Mdakuzi
Proudly Powered by Blogger.
back to top