Thursday, 23 August 2012

Muonekano Mpya wa Snoopy

Posted at  07:57  |  in  Ismail.zbn

SNOOP Dogg ni miongoni mwa wanamuziki wakongwe ambao wameweza kushikilia hadhi za juu katika chati za muziki.
Hivi karibuni Snoop  aliwaacha mashabiki wake vinywa wazi baada ya kutangaza rasmi kuachana na aina hiyo ya muziki na kuhamia kwenye Reggae.
Snoop ambaye anajulikana kupitia nyimbo zake zilizofanya vizuri kama  Beautiful, na Drop It Like It's Hot ametangaza uamuzi huo sambamba na jina lake jipya ambapo sasa  si snoop dogg bali ataitwa Snoop Lion.
Akitangaza hatua hiyo mbele ya waandishi wa habari nchini Jamaica Snoop, anasema ziara yake nchini humo ndiyo imemfanya kufikia maamuzi hayo baada ya kuhisi amezaliwa upya kwani sasa anataka kufanya muziki ambao utasikilizwa na watu wa kila rika.
Anasema kwa sasa ameamua kujikita katika muziki huo kwa sababu ya kuvutiwa na imani ya rasta na amechukua nafasi ya muhasisi wa reggae duniani  hayati Bob Marley anaamini kwamba anakila chembechembe za msanii huyo na hataki kabisa kuja kuacha tamaduni hiyo ya kirastafari.
“Siku zote nimekuwa nikitembea na roho ya Bob Marley na kwa sasa nimeingia rasmi kwenye reggae kuchukua nafasi yake kuuendeleze muziki huu nahitaji siku moja hata nikifa nikumbukwe kama ‘jah’,”anasema Snoop.
Anasema kwa muda wa siku 35 alizokuwepo nchini Jamaica amejikuta akijisikia kuhamia kwenye muziki ambao utasikilizwa na kila mtu katika familia yake tofauti na ilivyokuwa hapo awali akiimba rap.
Anaongeza kuwa ameamua kupumzika kuimba hip hop kwa kuwa amechoshwa na aina hiyo ya muziki pia hakuna changamoto anayokutana nayo kwa  kuwa anaumudu vyema na hakuna wa kusumbua kichwa chake katika eneo hilo.
Snoop Lion ameshatambulisha albamu yake ya kwanza katika miondoko hiyo itakayoitwa ‘Reincarneted fall in the fall’ ambayo itafuatiwa na jarida litakalojulikana kwa jina hilohilo.
Snoop Dogg ni nani?
Msanii huyu ambaye jina lake halisi ni Calvin Broadus alizaliwa Oktoba 20, 1971 karibu na  fukwe za mji wa  California. Alipata jina la utani la "Snoop" kutoka kwa mama yake kwa kuwa alikuwa alimfananisha mtoto wake huyo na muigizaji mmoja wa kipindi cha katuni.
Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari Snoop alikamatwa na polisi zaidi ya mara moja kutokana na kujihusisha na dawa za kulevya ambapo alijikuta akitupwa gerezani mara kadhaa.
Alifanikiwa kukutana na rapa  maarufu Dr. Dre ambaye alimuingiza kwenye muziki na kufanikiwa kutopa albamu yake ya kwanza mwaka 1993 iliyoitwa  Doggystyle ambayo ilifanya vizuri katika chati za muziki nchini Marekani.
Msanii huyu ni mtetezi mkubwa wa haki za watumiaji wa madawa ya kulevya aina ya marijuana hali iliyosababisha kuzuiwa kuingia nchini Norway baada ya kujaribu kubeba madawa hayo.
Imeandaliwa na Elizabeth Edward kwa msaada wa mtandao

Share this post

Kuhusu Mdaku Orijino

Tunafichua maovu, uozo na taka taka zoote wanazofanya watu wasio na staha. Unapicha yoyote habari yoyote ya washenzi wa tabia, tucheki tuwaanikeGoogle+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 BONGO MAGAZINE 1. by Mdakuzi
Proudly Powered by Blogger.
back to top