Kesho ni patashika nguo kuchanika,ni usemi maarufu inapotokea kuwa na mechio kali au jambo kubwa. Kwa wale wapenzi wa soka kesho liverpool and Manchester united watavaana kuwania pointi tatu muhimu katika uwanja wa Anfield mida ya saa tisa na nusu kwa masaa ya Africa mashariki, wakati huohuo Zipo taarifa za kuaminika ndani ya
Liverpool na Manchester United kuwa Wachezaji Luis Suarez na Patrice
Evra watapeana mikono kabla ya Mechi kati ya Timu hizo katika mpambano wa Ligi Kuu England.
Huku Mechi hiyo ikigubikwa na kumbukumbu
ya maafa yaliyotokea Mwaka 1989 wakati Mashabiki 96 wa Liverpool
walipofariki Uwanjani Hillsborough kwenye Mechi ya Nusu Fainali ya FA
Cup kati ya Liverpool na Nottingham Forest baada ya msongamano na
mkanyagano na Ripoti yake ya Uchunguzi kutolewa hivi juzi, Maafisa wa
Klabu hizi kubwa huko Uingereza ambazo zina uhasama wa jadi wamekutana
ili kupoza mlipuko wowote kwenye Mechi hiyo na hasa kutaka kuufuta
uhasama kati ya Wachezaji hao wawili baada ya Suarez kufungiwa kufuatia
kumkashifu kibaguzi Evra Msimu uliopita kwa kuwataka wapeana mikono.
Katika Mechi ya mwisho walipokutana, Suarez aligoma kupokea mkono wa Evra.
Tayari Meneja wa Manchester United, Sir
Alex Ferguson, ameshatamka kuisapoti Liverpool katika wakati wao mgumu
na Klabu hizi zimepanga kuikumbuka Siku hiyo ya Maafa ya Hillsborough
kwa Manahodha Steven Gerrard wa Liverpool na Nemanja Vidic wa Manchester
United kurusha Maputo 96 kabla Mechi kuanza ikiwa ishara ya kumbukumbu.
Pia Majukwaa ya Mashabiki yatapambwa na
Mabango ya Halaiki huku Jukwaa moja likiandika ‘Ukweli’, jingine likitoa
ishara ‘Haki’ na la tatu likisema ’96.’
Kuhusu hilo, Ferguson ametamka: “Itakuwa Siku ya kumbukumbu nzito. Tutawasapoti Liverpool kwa kila njia tunayoweza.”
0 comments: