Sunday 30 September 2012

Fergie Man utd haikua na bahati baada ya kupigwa 3-2 na spurs

Posted at  00:06  |  in  

Kwa mara ya kwanza tangu 1989, Tottenham wamefanikiwa kuifunga Manchester United bao 3-2 katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Old Trafford.Kocha huyo mzoefu wa ligi kuu england amesema timu yake haikua na bahati katika mchezo huo baada ya kosakosa nyingi.
Spurs walitangulia kupata bao mbili kwa kuisambaratisha Difensi ya Man United kwa kutumia kasi iliyoonyesha uzito wa Difensi hiyo kwa bao za Fulbeki Jan Vertonghen na ‘mkimbiaji’ Gareth Bale.
Bao hizo 2-0 zilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha Pili Man United walibadilika na kuonyesha wazi wazi hawakustahili kufungwa Mechi hii pale alipoingizwa Wayne Rooney na kumtengenezea Nani kufunga bao la kwanza lakini hapo hapo Spurs, wakidhirisha udhaifu wa Difensi ya Man United, wakapiga bao la tatu kupitia Clint Dempsey.
Shinji Kagawa aliifungia Man United bao la pili na waliendelea kutawala lakini walishindwa kupata bao la kusawazisha licha ya kosa kosa nyingi.
VIKOSI:
Manchester United: Lindegaard; Rafael, Ferdinand, Evans, Evra; Carrick, Scholes; Nani, Kagawa, Giggs; Van Persie.
Akiba: De Gea, Wootton, Anderson, Cleverley, Hernandez, Rooney, Welbeck.
Tottenham Hotspur: Friedel; Walker, Gallas, Caulker, Vertonghen; Sandro, Dembele; Lennon, Dempsey, Bale; Defoe.

Share this post

Kuhusu Mdaku Orijino

Tunafichua maovu, uozo na taka taka zoote wanazofanya watu wasio na staha. Unapicha yoyote habari yoyote ya washenzi wa tabia, tucheki tuwaanikeGoogle+.

0 comments:

About-Privacy Policy-Contact us
Copyright © 2013 BONGO MAGAZINE 1. by Mdakuzi
Proudly Powered by Blogger.
back to top