Naibu Waziri Wa Elimu Na Mafunzo Ya Ufundi nchini Tanzania
Mh. Philipo Augustino Mulugo, ameonyesha ukilaza na umbumbumbu wa hali
ya juu wakati akiwasilisha mada katika Mkutano wa Elimu na Ugunduzi kwa
nchi za Kiafrika.
Mkutano huo uliofanyika kuanzia tarehe 5 mpaka 7 mwezi Oktoba 2012
jijini Cape Town nchini Africa, uliwakusanyisha wataalamu mbalimbali wa
elimu na ufundi kutoka nchi za Kiafrika.
Tanzania ambayo kwenye mkutano huo mada yake iliwasilishwa na Mbunge
wa jimbo la Songwe ambaye pia ni Naibu Waziri Wa Elimu Na Mafunzo Ya
Ufundi Mh. Philipo Mulugo. Mada zote kwenye mkutano huo zilitakiwa
kuwasilishwa katika lugha ya Kingereza huku ikionekana dhahiri kabisa
juu ya uwezo mdogo katika uzungumzaji na usomaji wa lugha hiyo kwa
waziri huyo.
Naibu Waziri huyo ambaye alianza kujiumauma katika utambulishi wa
mada yake, aliboronga zaidi pale alisema kuwa Tanzania iliundwa baada ya
kuziunganisha nchi za Tanganyika na visiwa vya Zimbabwe na Pemba.
Ilitegemewa kwa mtu yeyote ambaye amefanya kosa kama hilo ni kuweza
kujisasahisha kwa haraka na kuwapa maelezo sahihi wajumbe katika mkutano
huo lakini haikuwa hivyo kwa Naibu Waziri huyo, kwani alionyesha
ukilaza na umbumbumbu wa hali ya juu kwa kuendelea na utoaji mada katika
mkutano huo.
Kitendo hicho ambacho kimewakasirisha na kuwatia aibu Watanzania
wengi hususani wale ambao ni watumiaji wa mitandao ya kijamii na blogu
mbalimbali. Watanzania wengi wamehoji ni kwa nini Naibu Waziri huyo
ambaye ameonyesha ana uwezo mdogo sana katika uwasilishaji mada
atawezaje kuhimili na kuwa dira na chachu katika maendeleo ya elimu
nchini Tanzania, je mtu kama huyu ni wa kutegemewa kuinua na kuleta
mapinduzi katika elimu.
Wakati umefika kwa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania kuteuwa viongozi ambao wana uwezo wa hali ya juu katika uendeshaji wa wizara mbalimbali.
Unaweza kuangalia video ya Mh. Philipo Mulugo wakati akiwasilisha mada hiyo katika hii blog.
0 comments: